• HABARI MPYA

  Saturday, August 20, 2022

  AZAM FC YASHUSHA PHYSIO MPYA KUTOKA URENO


  MTAALAMU wa tiba za wanamichezo, Joao Rodrigues amewasili usiku wa kuamkia leo kutoka kwao, Ureno kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Azam FC.
  Rodrigues ni physiotherapist wa viwango vya juu kwenye tiba za wachezaji, akiwahi kufanya kazi na mabingwa wa Ureno, FC Porto.
  Mkurugenzi wa Azam FC, Yusuf Bakhresa, kabla ya kuanza msimu huu aliahidi atawapa furaha mashabiki wa timu hiyo kwa kuleta wachezaji wa hali ya juu, kocha wa viungo, kocha wa makipa na sasa amemaliza kwa kushusha 'physio' wa viwango.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASHUSHA PHYSIO MPYA KUTOKA URENO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top