• HABARI MPYA

  Sunday, August 07, 2022

  YANGA YACHAPWA 2-0 NA MABINGWA WA UGANDA SIKU YA MWANANCHI

  WENYEJI, Yanga SC jana wamechapwa mabao 2-0 na mabingwa wa Uganda katika mchezo wa kirafiki kuhitimisha Siku ya Mwananchi na kwa ujumla Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dares Salaam.
  Mabao yaliyowazamisha nyumbani mabingwa wa Tanzania yalifungwa na Milton Karisa dakika ya kwanza tu na Anukani Bright dakika ya 64.
  Kikosi cha Yanga kinarejea kambini, Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Simba Agosti 13, yaani Jumamosi ijayo hapo hapo Uwanja wa Mkapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YACHAPWA 2-0 NA MABINGWA WA UGANDA SIKU YA MWANANCHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top