• HABARI MPYA

  Friday, August 12, 2022

  YANGA SC YAACHANA NA HASSAN BUMBULI BAADA YA KUMALIZA MKATABA

  UONGOZI wa klabu ya Yanga umeachana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli baada ya kumaliza mkataba wake.


  Kwa upande wake, Bumbuli ameushukuru uongozi wa Yanga kwa hatua hiyo akisema; “Kwa dhati  ya moyo Wangu NAWASHUKURU sana Wana Yanga, Hakika naweza kusema kwamba ni ninyi ndio mnafanya ukubwa huu Klabu ya Yanga,”. “Inaweza kuhuzunisha kwamba leo nawaaga, naondoka uongozini, lakini nina furaha na shauku kwa Changamoto mpya mbele yangu, na pia nina shauku kuona mpya yaliyoandaliwa kwa ajili yenu na kwa Klabu yangu pendwa,”.
  “Ni zawadi nzuri sana niliyopokea na kuifurahia kufanya kazi Yanga, kuwahudumia #Wananchi,”.
  “Ahsanteni kwa kunionyesha wema na hekima, hakika mlifanya Yanga kuwa mahali nilipofurahia sana kutumia muda wangu za kazi na zaidi,”.
  “Kwenu WanaYanga, sina la kusema, hii ni kwa sababu sipati maneno ya kuelezea jinsi ninavyowashukuru! Ninyi ni watu Maalum sana,”.
  “Nimekuja tukiwa watupu vyote pesa na mataji, naondoka huku vikapu vikiwa vimesheheni na rekodi iliyowekwa kwa kishindo. Ahsanteni kwa kunipa nafasi ya kuwatumikia,” amesema Bumbuli katika taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAACHANA NA HASSAN BUMBULI BAADA YA KUMALIZA MKATABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top