• HABARI MPYA

  Monday, August 15, 2022

  NAMUNGO NA MTIBWA HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MKAPA


  TIMU ya Namungo FC imelazimishwa sare ya 2-2 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Relliant Lusajo yote dakika ya 32 na 82, wakati ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Vedastus Mwihambi dakika ya 55 na Nickson Kibabage dakika ya 80.
  Namungo FC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kubeba pointi zote tatu baada ya Kassim Haruna kukosa penalti kipindi cha pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO NA MTIBWA HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top