• HABARI MPYA

  Saturday, August 13, 2022

  MAYELE APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA SIMBA 2-1 NA KUBEBA TENA NGAO


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya watani wa jadi, Simba SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Shujaa wa Yanga SC leo ni mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele aliyefunga mabao yote mawili kipindi cha pili baada ya winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho kuitanguliza Simba kipindi cha kwanza.
  Sakho alifunga bao zuri dakika ya 16 baada ya kuutokea vizuri mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama na kumtungua kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra.
  Kipindi cha pili Yanga ilizinduka na Mayele akafunga bao la kwanza dakika ya 50 akimalizia pasi ya kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki na la pili dakika ya 81 baada ya kuwachambua mabeki watatu wa Simba kufuatia pasi ya beki Dickson Job.
  Huu ni mwanzo mzuri mwingine kwa Yanga msimu baada ya msimu uliopita pia kuifunga Simba 1-0 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii bao la Mayele pia.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA SIMBA 2-1 NA KUBEBA TENA NGAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top