• HABARI MPYA

  Wednesday, August 31, 2022

  KOCHA KASEJA AKIWANOA MAKIPA WA TAIFA STARS KUIKABILI TENA UGANDA


  KOCHA mpya wa makipa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Juma Kaseja akiwaelekeza walinda mlango Aishi Manula, Abutwalib Mshery na Beno Kakolanya kwenye mazoezi jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Taifa Stars inajiandaa na mchezo wa marudiano na Uganda kufuzu Fainali za CHAN dhidi ya wenyeji, Uganda Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe. 
  Stars iliyofungwa 1-0 na The Cranes kwenye mchezo wa Jumapili Uwanja wa Mkapa. inahitaji ushindi wa 2-0 ili kufuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA KASEJA AKIWANOA MAKIPA WA TAIFA STARS KUIKABILI TENA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top