• HABARI MPYA

  Saturday, August 20, 2022

  PRISONS YAZINDUKA NA KUICHAPA DODOMA JIJI 2-1 LITI


  TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa LITI, zamani Namfua mjini Singida.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Ismail Mgunda dakika ya pili kwa penalti na Jeremiah Juma dakika ya sita, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 18.
  Ni ushindi wa kwanza kwa Prisons baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Singida Big Stars kwenye mechi ya kwanza, wakati kwa Dodoma Jiji ni kipigo cha pili baada ya kuchapwa 3-1 na Mbeya City hapo hapo LITI.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAZINDUKA NA KUICHAPA DODOMA JIJI 2-1 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top