• HABARI MPYA

  Saturday, August 20, 2022

  YANGA YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAICHAPA COASTAL 2-0 ARUSHA


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameendeleza mwanzo mzuri katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na winga Mghana, Bernard Morrison dakika ya nne na mtokea benchi, mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele dakika ya 68.
  Ni ushindi wa pili kwa Yanga baada ya kuichapa Polisi Tanzania 2-1 na kipigo cha kwanza kwa Coastal Union kufuatia kushinda 1-0 dhidi ya KMC kwenye mechi za kwanza hapo hapo Sheikh Amri Abeid.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAICHAPA COASTAL 2-0 ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top