• HABARI MPYA

  Thursday, August 25, 2022

  ZANZIBAR HEROES YAICHAPA THE CRANES 1-0 AMAAN


  BAO pekee la Ibrahim Mkoko limeipa Zanzibar Heroes ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda, The Cranes katika mchezo wa kirafiki usiku wa Jumatano Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mkoko alifunga bao hilo dakika ya 76 akimalizia pasi ya Abdulnasir Hassan Amal kutoka upande wa kulia.
  Uganda iliutumia mchezo huo kujiandaa na mechi dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kufuzu Fainali za CHAN Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
  Timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe na mshindi wa jumla atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZANZIBAR HEROES YAICHAPA THE CRANES 1-0 AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top