• HABARI MPYA

  Wednesday, August 31, 2022

  BOCCO AONGEZWA TAIFA STARS KUIVAA THE CRANES JUMAMOSI


  MSHAMBULIAJI wa mkongwe wa Simba SC, John Raphael Bocco ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kuelekea mchezo wa marudiano na Uganda kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Jumamosi Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe.
  Uteuzi huo umefanywa na makocha wapya wa muda, Mzambia Hanoor Janza na Msaidizi wake, Mecky Mexime na kocha wa makipa, Juma Kaseja siku mbili tu tangu wapewe jukumu hilo.
  Ikumbukwe juzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimuondoa kazini kocha Mdenmark, Kim Poulsen na wasaidizi wake kufuatia Taifa Stars kuchapwa 1-0 na Uganda katika mechi ya kwanza ya hatua hiyo ya mwisho ya mchujo wa kuwania  tiketi ya CHAN Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa  jumla atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO AONGEZWA TAIFA STARS KUIVAA THE CRANES JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top