• HABARI MPYA

  Wednesday, August 10, 2022

  FIFA YAAHIDI KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA


  RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Gianni Infantino amesema FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na kuridhishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Michezo.
  Akizungumza usiku wa kuamkia Agosti 10, 2022 mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa katika kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania.
  Akiongozana na wachezaji mahiri wazamani waliopata kucheza katika makombe ya dunia na mwamuzi Corina amesema amefurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania.
  "Tayari FIFA imekwishatoa msaada wa ujenzi wa viwanja changamani Dar na Tanga lakini wako tayari kwa ajili ya kuongeza vituo katika kanda nyingine" amefafanua Mhe. Mchengerwa
  Aidha, Mhe. Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa kwenye ambayo imesaidia Tanzania kupiga hatua duniani katika michezo.
  Mhe. Mchengerwa amepokea viongozi mbalimbali wa juu kwenye mashirikisho ya Soka duniani na kufanya vikao vya kuendeleza michezo ambao leo wanahudhuria mkutano Mkuu wa 44 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) jijini Arusha.
  Aidha, Mhe. Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuendelea kuimarisha mahusiano na mashirikiano na nchi mbalimbali ambazo tayari ziliahidi kuendeleza mashirikiano katika sekta za michezo, Sanaa na Utamaduni.
  Mkutano huu wa kihistoria unatarajiwa kuhudhuria na zaidi ya watu mia tano na waandishi wa habari zaidi ya mia moja huku ikitarajiwa kuangaliwa na zaidi ya watu bilioni moja.
  Tayari viongozi wakuu wa mashirikisho yote ya Soka kutoka mabara yote wamewasili na Waziri Mkuu, Mhe. Kasimu Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIFA YAAHIDI KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top