• HABARI MPYA

  Sunday, August 21, 2022

  AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA GEITA GOLD CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Azam FC ilitangulia kwa bao la chipukizi wake mwenye kipaji, Tepsie Evans dakika ya 41, kabla ya beki Adeyoum Ahmed kuisawazishia Geita Gold dakika ya 54.
  Ni sare ya kwanza kwa timu zote katika mechi mbili za mwanzo za msimu kufuatia Azam FC kushinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar hapo hapo Chamazi na Geita Gold kufungwa 3-0 na Simba Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA GEITA GOLD CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top