• HABARI MPYA

  Sunday, August 07, 2022

  SALAH AFIKIA REKODI YA ROONEY, LAMPARD NA SHEARER ENGLAND


  WENYEJI, Fulham wamelazimisha sare ya 2-2 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
  Mabao ya Fulham yamefungwa na Aleksandar Mitrović dakika ya 32 akimalizia pasi ya Kenny JoelleTete na lingine kwa penalti dakika ya 72, wakati ya Liverpool yamefungwa na Darwin Núñez dakika ya 64 na Mohamed Salah dakika ya 80.
  Mohamed Salah amefikia rekodi ya kufunga kwenye mechi za ufunguzi, hili likiwa bao la nane kwa mechi za kwanza za msimu sawa na magwiji wa England, Frank Lampard aliyewika Chelsea, Wayne Rooney aliyewika Manchester United na Alan Shearer aliyewika Newcastle United.
  Pia anashikilia rekodi ya kufunga mfululizo kwenye mechi za ufunguzi na bao lake hilo la 158 tangu aanze kuchezea Liverpool linamfanya afikie idadi ya mabao ya gwiji wa zamani wa klabu hiyo, Michael Owen. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH AFIKIA REKODI YA ROONEY, LAMPARD NA SHEARER ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top