• HABARI MPYA

  Friday, August 19, 2022

  YANGA YAINGIA MKATABA WA MASOKO NA JACKSON GROUP LTD


  KLABU ya Young Africans SC, Bingwa wa Ligi Kuu ya NBC , Kombe la Shirikisho la Azam kwa msimu wa 2021/2022 na bingwa wa ngao ya jamii Tanzania kwa mara ya pili mfululizo, imefanya makubaliano ya ubia wa kimasoko (marketing partnership) na Kampuni ya Jackson Group kwa kipindi cha miaka miwili.  
  Jackson Group ni kampuni ya kitanzania inayojihusisha na uwakala wa masoko nchini Tanzania na huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi wa haki za IP (IP rights management) pamoja na kufanya kazi na wadau wanaojihusisha na udhamini kwenye michezo wakiwa na uzoefu mkubwa wa kufanya kazi na wadhamini  wa ndani, Afrika na Ulaya.
  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said alisema,
  “Tunayo furaha kubwa kusaini mkataba huu na kampuni ya Jackson Group, kwa sababu inaenda kufungua milango ya kupata wadhamini na wadau ambao watatusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo ya klabu yetu, kwani tuna mipango na miradi mingi ambayo inahitaji ushirikiano wa namna hii”
  Akihudhuria hafla ya utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jackson Group Bw. Kelvin Twissa alisema, "Ni heshima kubwa kufanya kazi na mabingwa wa kihistoria Young Africans SC, uzoefu wetu wa ndani na wa kimataifa wa kurudushisha thamani ya uwekezaji kwa washirika wetu unaenda kuweka kiwango kipya katika kuwapa thamani wadhamini wetu. Tuna fursa nyingi kwa washirika wa ndani na wa kimataifa kuwa sehemu ya mafanikio ya Young Africans SC. Soka nchini Tanzania ina fursa nyingi  hata nje  ya masoko ya hapa ndani, tuna nia ya kukuza ushirikiano wa vilabu ili kuvutia washirika zaidi na kutoa thamani kwa washirika wetu wa sasa na wanaokuja”
  Young Africans SC walikuwa na msimu wa kipekee msimu uliopita kwa kushinda mataji matatu na imeanza msimu huu mpya kwa kutetea Ngao Ya Jamii huku wakionesha kiwango cha hali ya juu ikiwa na kikosi kipya cha msimu huu. Msimu mpya unatoa fursa kwa miradi mingi na ushirikiano ambao utaleta mapinduzi katika masoko ya michezo. katika ukanda huu.
  Mkataba huo umesainiwa leo hii tarehe 19 Agosti, mbele ya waandishi wa habari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAINGIA MKATABA WA MASOKO NA JACKSON GROUP LTD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top