• HABARI MPYA

  Sunday, August 28, 2022

  SIMBA QUEENS MABINGWA WA CECAFA 2022

  TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya She Corporates ya Uganda usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa kimataifa wa Kenya, Vivian Corazone Aquino Odhiambo dakika ya 49 kwa penalti baada ya Asha Djafar kuangushwa kwenye boksi na Simba Queen itauwakilisha ukanda wa CECAFA kwenye Ligi ya mabingwa ya wanawake Oktoba mwaka huu nchini Morocco.
  Pamoja na ushindi huo, Simba Queens pia wametoa kipa Bora wa mashindano, mzawa Gelwa Yona na Mchezaji Bora wa Mashindano, ambaye ni Vivian Corazone Aquino Odhiambo, huku Abela Roza wa Commercial Bank ya Ethiopia akiwa Mfungaji Bora.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS MABINGWA WA CECAFA 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top