• HABARI MPYA

  Monday, August 29, 2022

  TFF YAMFUTA KAZI KIM POULSEN TAIFA STARS


  SHIRIKISHO la Soka la Tanzania (TFF) limemuondoa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen kufuatia matokeo mabaya.
  Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Taifa Stars kuchapwa 1-0 na Uganda katika mechi ya kwanza Hatua ya mwisho ya mchujo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la The Cranes lililoizamisha Taifa Stars jana lilifungwa na Travis Mutyaba dakika ya 87 na sasa timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe na mshindi atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.
  Sasa kikosi kitakuwa chini ya kocha wa Namungo FC, Mzambia Hanoor Janza ambaye atasaidiwa na mzawa, Mecky Mexime huku Juma Kaseja akiwa kocha wa makipa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAMFUTA KAZI KIM POULSEN TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top