• HABARI MPYA

  Friday, August 05, 2022

  BONDIA MWINGINE WA TANZANIA AJIHAKIKISHIA MEDALI MADOLA


  BONDIA Kassim Suleiman Mbundwike ‘Mfupa wa Sokwe’ usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Ndondi Michezo wa Jumuiya ya Madola
  Inayoendelea Jijini Birmingham nchini England.
  Mbundwike ameingia Nusu Fainali baada ya kushinda Marion Faustino AH Tong wa Samoa kwa Refa Kusimamisha pambano hilo la uzito wa Light Middle (RSC) katika Raundi ya tatu.
  Kwa ushindi huo, Mbundwike amejihakikishia kupata medali ambayo itakua ya pili kwa upande wa Ngumi, na ya tatu kwa Team Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham.
  Mbundwike anajiunga na askari mwenzake wa JWTZ mwenye cheo kama yeye cha 'Private', Yusufu Changalawe, katika mpambano wa nusu fainali siku ya Jumamosi na kama wakishinda wataingia fainali Jumapili kugombea Medali za dhahabu na Fedha, wakiwa tayari wote wana medali za shaba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BONDIA MWINGINE WA TANZANIA AJIHAKIKISHIA MEDALI MADOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top