• HABARI MPYA

  Saturday, August 27, 2022

  LIVERPOOL YAIKANDAMIZA BOURNEMOUTH 9-0 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wameibamiza AFC Bournemouth mabao 9-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield na kupoza machungu ya kichapo cha 2-1 kutoka kwa mahasimu, Manchester United.
  Ushindi huo mnono umeifanya Liverpool ifikie rekodi ya kushinda mabao mengi kwenye mechi moja katika Ligi Kuu ya England iliyowekwa na Man United dhidi ya Ipswich mwaka 1994, Southampton mwaka 2021 na Leicester City kwa hao hao The Saints mwaka uliotangulia.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino na Luis Diaz mawili kila mmoja, Trent Alexander-Arnold, Harvey Elliott, Virgil van Dijk, Christopher Mepham aliyejifunga na Fabio Carvalho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAIKANDAMIZA BOURNEMOUTH 9-0 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top