• HABARI MPYA

  Thursday, August 25, 2022

  SIMBA QUEENS YATINGA FAINALI, KUKUTANA NA WAGANDA JUMAMOSI


  TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kwenda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya AS Kigali ya Rwanda usiku wa Jumatano Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Vivian Aquino Corazone dakika ya 14, Opa Clement Tukumbuke dakika ya 30, Aisha Juma Mnunka dakika ya 38 na Diana William Mnally dakika ya 84, wakati la AS Kigali limefungwa na Mukeshimana Dorothee dakika ya 28.
  Fainali ni Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
  Na Simba Queens itakutana na She Corporate ya Uganda ambayo imeitoa Commercial Bank ya Ethiopia kwa kuichapa 2-1 pia Jumatano jioni.
  Simba Queens na She Corporate ni marudio ya mchezo baina yao wa Kundi B ambao Malkia hao wa Msimbazi waliibuka na ushindi wa 2-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YATINGA FAINALI, KUKUTANA NA WAGANDA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top