• HABARI MPYA

  Saturday, August 27, 2022

  STERLING APIGA MBILI CHELSEA PUNGUFU YASHINDA 2-1


  WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Pongezi kwa mfungaji wa mabao yote hayo, mchezaji mpya, Raheem Sterling dakika ya 47 akimalizia pasi ya Marc Cucurella na 63 akimalizia pasi ya Reece James.
  Katika mchezo huo, Chelsea ilicheza pungufu tangu dakika ya 28 baada ya kiungo wake Conor John Gallagher kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
  Bao la kufutia machozi la Leicester City limefungwa na Harvey Lewis Barnes dakika ya 66 akimalizia pasi ya mkongwe, Jamie Richard Vardy.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STERLING APIGA MBILI CHELSEA PUNGUFU YASHINDA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top