• HABARI MPYA

  Tuesday, August 09, 2022

  NBC LUGALO PATRON TROPHY KUTIMUA VUMBI AGOSTI 27


  SHINDANO la Mchezo wa Golf la kumuenzi aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo "NBC Lugalo Patron Trophy" linatarajiwa kufanyika 27 Agosti 2022 katika viwanja vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Lugalo Dar es Salam
  Akizungumzia ujio wa shindano hilo Mwenyekiti wa Klabu Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luongo amesema,pia  Lengo la shindano hilo Ni kumkaribisha mlezi mpya wa klabu ambaye ni mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Jacob John Mkunda.
  Kwa upande wake mwakilishi kutoka Benki ya NBC ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo Mkurugenzi wa Wateja binafsi na Wateja Wadogo Ellibariki Masuke ameishukuru Klabu ya Lugalo Gofu kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo na amewaomba wadau na Watanzania wajitokeze kwa wingi katika shindano hilo.
  Benki ya NBC imekabidhi vifaa vya Mchezo  wa Gofu ambavyo vitatumika katika shindano hilo,"NBC Lugalo Patron Trophy'" linarotarajiwa kufanyika 27 Agosti 2022, ambapo mgeni rasmi katika ufungaji wa Shindano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa utamaduni,Sanaa na Michezo  Mohammed Mchengelwa.


  Mkurugenzi wa wateja binafsi kutoka benki ya Nbc Elibariki Masuke akizungumza mara baada ya kutambulishwa rasmi Kwa Shindano la ''NBC Lugalo patron trophy " lengo likiwa ni kumuaga aliyekua Mlezi wa Klabu ya jeshi ya Lugalo gofu Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo na kumkaribisha rasmi Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda linalotarajiwa kufanyika agosti 27 mwaka huu katika viwanja vya jeshi lugalo gofu Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NBC LUGALO PATRON TROPHY KUTIMUA VUMBI AGOSTI 27 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top