• HABARI MPYA

  Monday, August 29, 2022

  AZAM FC YAWAONDOA MAKOCHA WASOMALI WOTE WAWILI


  KLABU ya Azam FC imeondoa kazi makocha wake wawili, Wamarakani wenye asili ya Somalia, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser.
  Taarifa ya Azam FC imesema; “Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi mtawalia.
  Hata hivyo, Azam imesema makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye.
  Sasa Azam FC inabaki chini ya makocha Waspaniola, Dani Cadena kocha wa makipa, Mikel Guillen kocha wa Fiziki 
  na mtaalamu wa tiba za wanamichezo (physio), Mreno Joao Rodrigues.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWAONDOA MAKOCHA WASOMALI WOTE WAWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top