• HABARI MPYA

  Tuesday, August 16, 2022

  MABINGWA YANGA WABEBA POINTI TATU ZA KWANZA LIGI KUU UGENINI


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi kwa Watoto wa Jangwani, kwani walilazimika kutoka nyuma baada ya Polisi kutangulia kwa bao la Salum Ally Kipemba dakika ya 34.
  Bao hilo lilikuja baada ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fiston Kalala Mayele kukosa penalti dakika ya 11 tu ya mchezo.
  Alikuwa ni Mayele mwenyewe aliyefuta makosa yake kwa kuifungia Yanga bao la kusawazisha dakika ya 41, kabla ya Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto naye kufuta makosa yake yaliyosababisha bao la Polisi kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 84.
  Polisi ilimaliza pungufu baada ya nyota wake, Ally Othman Mmanga kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 88 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABINGWA YANGA WABEBA POINTI TATU ZA KWANZA LIGI KUU UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top