MORRISON NA BIGIRIMANA WAFUNGA YANGA YAICHAPA KMC 2-1 KIGAMBONI
MABINGWA wa Tanzania, Yanga jana wameichapa KMC 2-1 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Avic Town, Somangira, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na winga Mghana, Bernard Morrison na kiungo Mrundi, Gael Bigirimana, wakati la KMC limefungwa na Sadallah Lipangile.
0 comments:
Post a Comment