• HABARI MPYA

  Friday, August 26, 2022

  SIMBA SC WAENDA SUDAN KUCHEZA NA KOTOKO NA HILAL


  KIKOSI cha Simba SC kimendoka Ijumaa Alfajiri ya leo kwenda Sudan kushiriki michuano maalum ya timu tatu, kwa mwaliko wa wenyeji, El Hilal.
  Simba imeondoka na wachezaji 19 klabu ya Simba, tisa wakibaki na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda kufuzu Fainali za CHAN na kiungo Sadio Kanoute jana ameenda nyumbani kwao Mali kwa ajili ya kushughulikia hati ya kusafiria.
  Wachezaji 19 waliosafiri na Simba kwenda Sudani ni makipa Ally Salim, Ahmed Ferouz, mabeki Israel Mwenda, Gardiel Michael, Henock Inonga, Mohamed Ouattara, Joash Onyango na Easto Nyoni.
  Wengine ni viungo Victor Akpan, Nassoro Kapama, Clatous Chama, Nelson Okwa, Peter Banda, Jimmyson Mwanuke, Pape Sakho, Augustine Okrah na washambuliaji Moses Phiri, John Bocco na Dejan Georgijevic.   
  Ikiwa huko, Simba itamenyana na Asante Kotoko ya Ghana Jumapili kabla ya kumalizana na wenyeji, El Hial Jumatano ijayo, Agosti 31 kisha watarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Djibouti, AS Arta Solar.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAENDA SUDAN KUCHEZA NA KOTOKO NA HILAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top