• HABARI MPYA

  Sunday, May 01, 2022

  LIVERPOOL YAICHAPA NEWCASTLE 1-0 ST. JAMES' PARK


  BAO la kiungo Mgunea, Naby Laye Keïta dakika ya 19 akimalizia pasi ya Mreno, Diogo Jota limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa St. James' Park, Newcastle.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 82, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 34, wakati Newcastle inabaki na pointi zake 43 za mechi 35 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA NEWCASTLE 1-0 ST. JAMES' PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top