• HABARI MPYA

    Thursday, July 01, 2021

    KMC YAAMUA MECHI YAO YA LIGI KUU DHIDI YA SIMBA SC WACHEZEE BENJAMIN MKAPA BADALA YA CCM KIRUMBA

    MCHEZO wa Ligi Tanzania Bara Kati ya timu ya KMC dhidi ya Simba utakaofanyika Julai 7, utachezwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, badala ya Uwanja wa CCM Kirumba uliopo  mkoani Mwanza. 
    Ofisa Habari wa KMC Christina Mwaigala, Alisema kuwa Uongozi wao umewasilisha barua bodi ya ligi Tanzania TPLB kuomba mchezo huo sasa uchezwe dar es Salaam badala ya Kirumba.
    Alisema kuwa upande waaandalizi ya timu yao inaendelea kujifua chini ya Kocha Mkuu, John Simkoko na Msaidizi, Habib Kondo kwa lengo la kuhakikisha kwamba Timu inakwenda kupata matokeo mazuri.


    Mwaigala alisema licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa katika mchezo huo lakini uongozi pamoja na wachezaji umedhamiria kupata alama tatu kwakuwa KMC FC haijawahi kushindwa na kwamba itahakikisha ushindi huo unapatikana ili kuendelea kujiweka katika hatua nzuri ya kuendelea kuwania nafasi ya Nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu 2020/2021.
    “Tunafahamu mchezo huu utakuwa na ushindani mkubwa sana, kutokana na Timu ambayo tunakutana nayo imekuwa ikifanya vizuri, lakini Makocha wetu wanaendelea kukiweka vizuri kikosi cha wana Kino Boys kuwa bora kwa maana ya kupata alama tatu, nakumaliza kwenye nafasi nzuri, hivyo hatuna wasiwasi na mchezo huo kikubwa tunajenga tahadhari ikiwa ni pamoja na kuendelea kujiweka vizuri kabla ya Julai saba.
    Katika hatua nyingine KMC FC jana imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Timu ya Pamba ya Mkoani Mwanza katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kupata ushindi wa magoli mawili kwa sifuri ambayo yamefungwa na wachezaji Kevin Kijili pamoja na Crifu Buyoya ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujiweka sawa katika mchezo dhidi ya Simba.
    KMC FC kwa sasa imesalia na micheo mitatu kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ambayo ni dhidi ya Simba, JKT Tanzania pamoja na Ihefu huku ikiwa imecheza michezo 31 na kujikusanyia jumla ya alama 42.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KMC YAAMUA MECHI YAO YA LIGI KUU DHIDI YA SIMBA SC WACHEZEE BENJAMIN MKAPA BADALA YA CCM KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top