• HABARI MPYA

  Thursday, July 15, 2021

  KAGERE AIFUNGIA BAO LA KUSAWAZISHA SIMBA SC BADO DAKIKA TANO YALAZIMISHA SARE YA 1-1 NA AZAM FC LEO CHAMAZI

  MABINGWA wa Simba SC wamelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Azam FC walitangulia kwa bao la kiungo wake mshambuliaji mahiri Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 43, kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere akaifungia Simba SC bao la kusawazisha dakika ya 85.
  Simba SC, ambao ni mabingwa tayari kwa mara ya nne mfululizo wanafikisha ponti 80 baada ya sare hiyo na sasa wanawazidi watani wa jadi, Yanga SC pointi saba kuelekea mechi za mwisho za msimu Jumapili na watamaliza na Namungo, siku ambayo watakabidhiwa Kombe lao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERE AIFUNGIA BAO LA KUSAWAZISHA SIMBA SC BADO DAKIKA TANO YALAZIMISHA SARE YA 1-1 NA AZAM FC LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top