WACHEZAJI wa Simba SC wakifurahia na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC, bao la kiungo Mganda, Thadeo Lwanga dakika ya 80 jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Ni taji la pili mfululizo la ASFC kwa Simba SC na taji la tatu la msimu, baada ya kubeba Ngao ya Jamii na ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mapema mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment