• HABARI MPYA

  Thursday, July 22, 2021

  AZAM FC YAENDELEA KUIMARISHA KIKOSI CHAKE KUELEKEA MSIMU UJAO, YAMSAJILI NA KIUNGO WA KIMATAIFA WA KENYA, KENNETH MUGUNA


  KLABU ya Azam FC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Kenneth Muguna, kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Gor Mahia ya kwao.
  Muguna ambaye mkataba huo utamfanya aitumikie Azam FC hadi mwaka 2023 ni miongoni mwa nyota wanaotamba kwenye soka la Kenya, msimu huu akifanikiwa kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Kombe la FA la nchini huko, iliyomalizika kwa timu yake ya Gor Mahia kuibuka mabingwa wa michuano hiyo.
  Huyo anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa Azam FC kuelekea msimu ujao, baada ya nyota wawili kutoka Zambia, Charles Zulu, Rodgers Kola na beki mzawa wa kushoto, Edward Manyama.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAENDELEA KUIMARISHA KIKOSI CHAKE KUELEKEA MSIMU UJAO, YAMSAJILI NA KIUNGO WA KIMATAIFA WA KENYA, KENNETH MUGUNA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top