• HABARI MPYA

  Sunday, July 25, 2021

  THADEO LWANGA AWAZIMA YANGA SC KIGOMA, SIMBA SC YATWAA TENA TAJI LA AZAM SPORTS FEDERATION CUP


  SIMBA SC wamefanikiwa kutetea Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa kimafaifa wa Uganda, Thadeo Lwanga dakika ya 80 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimafaifa wa Msumbiji, Jose Luis Miquissone.
  Yanga ililazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 45 na ushei baada ya kiungo Mkongo, Tonombe Mukoko kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco.
  Ni taji la pili mfululizo la ASFC kwa Simba SC na taji la tatu la msimu, baada ya kubeba Ngao ya Jamii na ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mapema mwezi huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: THADEO LWANGA AWAZIMA YANGA SC KIGOMA, SIMBA SC YATWAA TENA TAJI LA AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top