• HABARI MPYA

  Monday, July 12, 2021

  ITALIA WAIZIMA ENGLAND KWA MATUTA WEMBLEY NA KUBEBA EURO 2020

   ITALIA imefanikiwa kutwaa taji la Euro 2020 baada ya ushindi wa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 usiku huu Uwanja wa Wembley Jijini London.
  England walitangulia kwa bao la nyota wa Manchester United, Luke Shaw dakika ya pili tu, kabla ya beki mwenzake, Leonardo Bonucci wa Juventus kuisawazishia Italia dakika ya 67.
  Wachezaji wote wa England walioingia mwishoni mwa mchezo kwa ajili ya kupiga penalti walikosa, Marcus Rashford akigongesha mwamba na mkwaju wa Jadon Sancho ukipanguliwa na kipa wa AC Milan, Gianluigi Donnarumma.


  Mwingine aliyekosa penalti upande wa England ni beki wa Arsenal, Bukayo Saka ambaye yake pia iliokolewa, wakati kipa  wa Everton, Jordan Pickford alipangua mikwaju ya mshambuliaji wa Torino, Andrea Belotti na kiungo Jorgingo Filho wa Chelsea.
  Waliofunga penalti za Italia ni Domenico Berardi wa Sassuolo, Bonucci na Federico Bernardeschi wa Juventus, wakati walioifungia England ni Harry Kane wa Tottenham Hotsour na Harry Maguire wa Manchester United.
  Hilo linakuwa taji la pili la Euro kwa Azzuri baada ya awali kulibebea nyumbani mwaka 1968 walipoifunga Yugoslavia 2-0 katika fainali Uwanja wa Olimpico Jijini Roma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ITALIA WAIZIMA ENGLAND KWA MATUTA WEMBLEY NA KUBEBA EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top