• HABARI MPYA

  Saturday, July 24, 2021

  TANZANIA YATINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA CECAFA U23 BAADA YA SARE YA 1-1 NA UGANDA LEO NCHINI ETHIOPIA

  TANZANIA imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 23 (CECAFA Challenge U23) baada ya sare ya 1-1 na Uganda leo Uwanja wa Bahir Dar nchini Ethiopia.
  Tanzania ilianza kupata bao dakika ya 32 kwa penalti kupitia kwa beki wa kulia, Israel Patrick Mwenda, kabla ya Uganda kusawazisha kupitia kwa Steven Mkwala dakika ya 40.
  Kipa wa Tanzania, Metacha Mnata ameibuka shujaa baada ya kuwanyima bao Uganda kwa kuokoa mkwaju wa penalti kipindi cha kwanza katika mchezo huo wa Kundi A.
  Tanzania inatinga Nusu Fainali baada ya kukusanya pointi nne kwenye mechi mbili, kufuatia kuichapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kundi hilo Jumanne na itamenyana na Sudan Kusini Jumanne wakati Burundi itamenyana na Kenya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YATINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA CECAFA U23 BAADA YA SARE YA 1-1 NA UGANDA LEO NCHINI ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top