• HABARI MPYA

  Tuesday, July 06, 2021

  BRAZIL YATINGA FAINALI COPA AMERICA, YAISUBIRI ARGENTINA

  TIMU ya taifa ya Brazil imefanikiwa kutinga fainali ya Copa America baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Peru katika mchezo wa Nusu Fainali usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Nilton Santos Jijini Rio de Janeiro.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Lyon ya Ufaransa, Lucas Paquetá dakika ya 35 akimalizia pasi ya nyota mwenzake wa Ligue 1, Neymar wa PSG.
  Brazil sasa itakutana na mshindi kati ya Argentina na Colombia zinazomenyana usiku wa kuamkia kesho na fainali itachezwa Jumapili.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRAZIL YATINGA FAINALI COPA AMERICA, YAISUBIRI ARGENTINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top