• HABARI MPYA

  Wednesday, July 07, 2021

  MUGALU APIGA ZOTE SIMBA SC YAICHAPA KMC 2-0 NA KUWEKA MKONO MMOJA KWENYE TAJI LA NNE MFULULIZO LA LIGI KUU

  MSHAMBULIAJI Mkongo, Chris Kope Mutshimba Mugalu amefunga mabao yote leo, Simba SC ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mugalu alifunga mabao yake yote kwa usaidizi wa viungo wa Zambia, la kwanza dakika ya tatu ya mchezo akimalizia pasi ya Clatous Chama na la pili dakika ya 45 akimalizia pasi ya Rally Bwalya.
  Kwa ushindi huo, Simba SC wanafikisha pointi 76 baada ya kucheza mechi 31, sita zaidi ya Yanga inayofuatia ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.


  Na sasa Wekundu wa Msimbazi watahitaji hata sare Jumapili dhidi ya Coastal Union hapo hapo Mkapa ili kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya nne mfululizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUGALU APIGA ZOTE SIMBA SC YAICHAPA KMC 2-0 NA KUWEKA MKONO MMOJA KWENYE TAJI LA NNE MFULULIZO LA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top