SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema litagawa barakoa kwa kila shabiki atakayeingia Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma kesho kushuhudia fainali ya Azam Sports Federation Cuo (ASFC).
Tamko hilo la TFF linafuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima mkoani humo ili kujihadhari na maambukizi ya virusi vya corona.
Andengenye amewataka watazamaji watakaoingia Uwanja wa Lake Tanganyika kesho kuzingatia tahadhari za maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19 kwa kuvaa barakoa.
0 comments:
Post a Comment