• HABARI MPYA

  Wednesday, July 14, 2021

  UEFA YATAJA KIKOSI BORA CHA EURO 2021 BILA CRISTIANO RONALDO

  UEFA imetaja muunganiko wa wachezaji wa kuunda kikosi Bora Euro 2020, lakini ajabu Mfungaji Bora, Cristiano Ronaldo hayumo.
  Kutoka England iliyofungwa na Italia katika fainali kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 Jumapili imetoa wachezaji watatu ambao ni Raheem Sterling, Harry Maguire na Kyle Walker.
  Kwa upande wao, mabingwa Azzurri wametoa wachezaji watano ambao ni Gianluigi Donnarumma, Leonardo Bonucci, Leonardo Spinazzola, Jorginho na Federico Chiesa.
  Timu nyingine zimetoa mchezaji mmoja mmoja ambazo ni Ubelgiji, Romelu Lukaku, Denmark, Pierre Emile-Hojbjerg na Hispania imemtoa Pedri pekee.


  KIKOSI CHA UEFA CHA MASHINDANO:
  Gianluigi Donnarumma (Italia), Kyle Walker (England), Leonardo Bonucci (Italia), Harry Maguire (England), Leonardo Spinazzola (Italia), Jorginho (Italia), Pierre-Emile Hojbjerg (Denmark), Pedri (Hispania); Federico Chiesa (Italia), Romelu Lukaku (Ubelgiji) na Raheem Sterling (England).

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UEFA YATAJA KIKOSI BORA CHA EURO 2021 BILA CRISTIANO RONALDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top