• HABARI MPYA

    Saturday, July 31, 2021

    AZAM FC YAMSAJILI MSHAMBULIAJI MKONGO, IDRIS MBOMBO KUTOKA EL GOUNAH YA MISRI KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI


    KLABU ya Azam FC imemsainisha mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo, kutoka El Gounah ya Misri.
    Mbombo amesaini mkataba huo mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya kuhudumu ndani ya timu yetu hadi mwaka 2023.
    Mshambuliaji huyo hatari, aliyewahi kuzichezea kwa mafanikio timu za Nkana, Zesco United, Kabwe Warriors, zote za Zambia, anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo msimu uliopita ililtegemea zaidi Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo.


    Huyo anakuwa mchezaji mpya wa sita dirisha hili kubwa la usajili baada ya Mkenya, Kenneth Muguna, Wazambia watatu, Charles Zulu, Paul Katema,  mshambuliaji Rodgers Kola na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAMSAJILI MSHAMBULIAJI MKONGO, IDRIS MBOMBO KUTOKA EL GOUNAH YA MISRI KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top