• HABARI MPYA

  Wednesday, July 21, 2021

  CHIPUKIZI MTANZANIA KELVIN JOHN AFUNGA BAO KRC GENK IKIIBUKA NA USHINDI WA 5-2 MECHI YA KIRAFIKI UBELGIJI

   MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Kelvin John Pius jana ameifungia klabu yake, KRC Genk bao moja katika ushindi wa 5-2 dhidi ya MVV kwenye mchezo wa kirafiki Uwanja wa B-Veld Racing Genk Jijini Genk, Ubelgiji.
  Katika mchezo huo wa kujiandaa na msimu, mabao mengine ya Genk yalifungwa na Cyriel Dessers mawili na Luca Oyen na Sekou Diawara moja kila mmoja.
  Kelvin mwenye umri wa miaka 18, alijiunga na timu hiyo Juni mwaka huu kutoka akademi ya Brook House Collage ya England kwa mkataba wa hadi mwaka 2024.


  Mchezaji wa zamani wa Genk, Mtanzania mwenzake, Mbwana Ally Samatta ndiye aliyefanikisha mpango wa klabu hiyo chipukizi huyo.
  Kelvin alijiunga na akademi ya Brook House Collage mwaka 2019 baada ya kung'ara kwenye Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17.
  Samatta, Nahodha wa Taifa Stars mwenye umri wa miaka 28 sasa, alipita Genk kwa miaka minne kuanzia 2016 kabla ya kwenda Aston Villa ya England mwaka 2020 ambayo baada ya miezi kadhaa ilimtoa kwa mkopo Fenerbahce ya Uturuki anakocheza hadi sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIPUKIZI MTANZANIA KELVIN JOHN AFUNGA BAO KRC GENK IKIIBUKA NA USHINDI WA 5-2 MECHI YA KIRAFIKI UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top