• HABARI MPYA

  Wednesday, July 21, 2021

  ANTETOKOUNMPO AIPA BUCKS UBINGWA WA NBA BAADA YA MIAKA 50

  MBELGIJI Giannis Antetokounmpo ameiongoza Milwaukee Bucks kutwaa taji la kwanzw la NBA ndani ya miaka 50 baada ya ushindi wa 105-98 dhidi ya Phoenix Suns kwenye mechi ya sita kati ya saba za fainali ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani.
  Baada ya kupoteza mechi mbili za kwanza za fainali, Bucks ikazinduka na kushinda zote nne zilizofuata na kutwaa taji mbele ya mashabiki wao nyumbani Alfajiri ya leo.
  MVP huyo mara mbili, Antetokounmpo amefunga pointi 50 na rebounds 14 kuipa Bucks taji la pili tu kihistoria la NBA baada ya lile walilochukua mwaka 1971.


  Kwa kazi hiyo nzuri, haikushangaza nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alipotangazwa MVP wa fainali akiingia kwenye orodha ya wachezaji saba tu kuwahi kufunga pointi 50 kwenye mechi za mwisho za fainali za NBA.
  Antetokounmpo pia alifanya blocks tano za hatari kwenye mechi hiyo iliyochezwa mbele ya mashabiki 17,000 ukumbi wa Fiserv Forum, huko Milwaukee, Wisconsin, wakati Chris Paul aliongoza kufunga upande wa Suns kwa pointi zake 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ANTETOKOUNMPO AIPA BUCKS UBINGWA WA NBA BAADA YA MIAKA 50 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top