• HABARI MPYA

  Tuesday, July 27, 2021

  SPURS YAMSAJILI KIUNGO BRYAN GIL KUTOKA SEVILLA

  KLABU ya Tottenham Hotspur imekamilisha usajili wake wa kwanaa kwa kumnyakua Bryan Gil kutoka Sevilla kwa ada ya Pauni Milioni 22.
  Pamoja na dau hilo, Spurs imemtoa nyota wake, Erik Lamela kwenda upande wa pili.
  Gil ni mchezaji wa pili kusajiliwa Spurs dirisha hili baada ya kipa, Pierluigi Gollini kwa mkopo kutoka Atalanta.
  Lakini Gil hatajiunga na kikosi cha Spurs hivi sasa, kwa sababu kiungo huyo yupo na kikosi cha Hispania kwenye Michezo ya Michezo ya Olimpiki. 


  Na kuwasili kwake kunafungua milango ya mchezaji wa muda mrefu Tottenham, Lamela kutimkia Sevilla baada ya miaka minane ya kuwa na timu hiyo ya London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SPURS YAMSAJILI KIUNGO BRYAN GIL KUTOKA SEVILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top