• HABARI MPYA

  Saturday, July 24, 2021

  AZAM FC YAWAACHA NYOTA WAKE WANNE WA KIGENI, CHIRWA, MPIANA MONZINZI, YAKUBU NA ALLY NIYONZIMA

  KLABU ya Azam FC imewaacha wachezaji wake wanne wa kigeni baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
  Hao ni beki wa kati, Mghana Yakubu Mohammed, kiungo Mnyarwanda Ally Niyonzima na washambuliaji Mkongo Mpiana Monzinzi na Mzambia Obrey Chirwa, ambaye pekee mkataba wake umemalizika.
  "Azam FC tunawashukuru kwa mchango wao waliotoa katika klabu hii bora kipindi chote walichokuwa nasi na tunawatakia kila la kheri huko waendako," imesema taarifa ya Azam FC leo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWAACHA NYOTA WAKE WANNE WA KIGENI, CHIRWA, MPIANA MONZINZI, YAKUBU NA ALLY NIYONZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top