• HABARI MPYA

  Tuesday, July 13, 2021

  TANZANIA YAPANGWA KUNDI A CECAFA CHALLENGE U23 ETHIOPIA 2021 PAMOJA NA UGANDA NA DRC

  TANZANIA imepangwa Kundi A katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 23, CECAFA Challenge U23 inayotarajiwa kufanyika Ethiopia baadaye mwezi huu.
  Tanzania imepangwa pamoja na Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wenyeji, Ethiopia wapo Kundi B pamoja na Burundi na Eritrea.
  Kundi C linazikutanisha U23 za Kenya, Sudan Kusini na Djibouti katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 18 hadi 30, mwaka huu.
  Vinara wa makundi yote wataingia Nusu Fainali pamoja na timu itakayomaliza na wastani mzuri zaidi katika nafasi ya pili.


  MAKUNDI;
  Kundi A: Uganda, Tanzania, DRC
  Kundi B: Ethiopia, Burundi, Eritrea
  Kundi C: Djibouti, Sudan Kusini, Kenya

  RATIBA
  Julai 18: Uganda vs DRC
  Ethiopia vs Eritrea Julai 19; Djibouti vs Kenya Julai 21; Burundi vs Eritrea
  Julai 22; Sudan Kusini vs Kenya
  Tanzania vs DRC
  Julai 24; Ethiopia vs Burundi
  Julai 25; Djibouti vs Sudan Kusiji
  Uganda vs Tanzania
  NUSU FAINALI
  Julai 28; Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Pili Bora
  Mshindi Kundi B vs Mshindi Kundi C
  FAINALI - Julai 30
  MSHINDI WA TATU - Julai 30
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAPANGWA KUNDI A CECAFA CHALLENGE U23 ETHIOPIA 2021 PAMOJA NA UGANDA NA DRC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top