• HABARI MPYA

  Saturday, July 10, 2021

  RAMOS ATUA PSG BAADA YA KUKATAA OFA YA ARSENAL

  KLABU ya Paris Saint-Germain imemsajili beki Sergio Ramos baada ya kuondika Real Madrid kama mchezaji huru kufuatia kumaliza mkataba.
  Ramos ameondoka Real Madrid baada ya kumaliza mkataba na pamoja na ofa za klabu kadhaa Ulaya Ikiwemo Arsenal, lakini ameamua kwenda Ufaransa.
  Beki huyo mkongwe wa kati amesaini mkataba wa miaka miwili kupiga kazi Parc des Princes na atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni Milioni 10.3 kwa msimu ambayo ukiongeza posho itafika Pauni Milioni 13.
  Baada ya kusaini mkataba huo, mkongwe huyo wa Hispania akasema; “Nina furaha kujiunga na Paris Saint-Germain,”.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAMOS ATUA PSG BAADA YA KUKATAA OFA YA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top