• HABARI MPYA

  Wednesday, July 07, 2021

  NYOTA WA CRYSTAL PALACE, CHRISTIAN BENTEKE AJA TANZANIA KUJIFARIJI BAADA YA UBELGIJI KUTOLEWA EURO 2020

  MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace ya England, Christian Benteke yuko nchini Tanzania kwa Mapumziko baada ya Ubelgiji kutolewa kwenye michuano ya Euro 2020.
  Benteke alionekana akipiga picha na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) katika lango kuu la kuingia katika hifadhi hiyo.
  Ujio wa mchezaji huyo mzaliwa wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unakuja wakati shughuli za utalii zimeboreshwa nchini jambo ambalo linaendelea kusisitiza kuwa Tanzania ni salama kwa ajili ya shughuli za utalii kwa wageni.


  Benteke anakuja nchini siku tatu tu baada ya Ubelgiji kutolewa kwenye michuano ya Euro 2020 baada ya kufungwa 2-1 na Italia katika Robo Fainali.
  Benteke ni miongoni mwa wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha Ubelgiji kwenye michuano hiyo inayoendelea ikiwa imefika katika hatua ya Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYOTA WA CRYSTAL PALACE, CHRISTIAN BENTEKE AJA TANZANIA KUJIFARIJI BAADA YA UBELGIJI KUTOLEWA EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top