• HABARI MPYA

  Monday, July 19, 2021

  BOCCO AWA MFUNGAJI BORA WA KWANZA MZAWA LIGI KUU BAADA YA WAGENI KUTAWALA MIAKA MITATU MFULULIZO

  MSHAMBULIAJI na Nahodha wa Simba amibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2020-2021 akiiwezesha klabu kutwaa taji la nne mfululizo.
  Bocco amemaliza msimu na mabao 16, akifuatiwa na wageni, Mkongo Chris Kope Mugalu 15 na Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo 14.
  Bocco anakuwa mfungaji bora wa kwanza mzawa tangu Simon Msuva alipochukua kwa pamoja na Abrhaman Mussa mwaka 2017.
  Baada ya hapo ni wageni waliotawala, Mganda Emmanuel Okwi 2018 na Mnyarwanda Meddie Kagere mara mbili mfululizo 2019 na 2020.


  ORODHA YA WAFUNGAJI BORA TANGU 2010:
  2010: MUSSA MGOSI (SIMBA SC) MABAO 18
  2011: MRISHO NGASSA (AZAM) MABAO 18
  2012: JOHN BOCCO (AZAM) MABAO 19 
  2013: AMISI TAMBWE  (SIMBA SC) MABAO 19
  2014: KIPRE TCHETCHE (AZAM FC) MABAO 17 
  2015: SIMON MSUVA (YANGA SC) MABAO 17
  2016: AMISI TAMBWE (YANGA SC) MABAO 21
  2017: SIMON MSUVA (YANGA SC) NA ABRAHMAN MUSSA (RUVU SHOOTING )MABAO 14
  2018: EMANUEL OKWI (SIMBA SC) MABAO 20
  2019: MEDDIE KAGERE MABAO 23
  2020: MEDDIE KAGERE (SIMBA SC) MABAO 22
  2021: JOHN BOCCO (SIMBA SC) MABAO 16
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO AWA MFUNGAJI BORA WA KWANZA MZAWA LIGI KUU BAADA YA WAGENI KUTAWALA MIAKA MITATU MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top