• HABARI MPYA

  Friday, July 09, 2021

  MSHAMBULIAJI WA POLISI TANZANIA AVUNJIKA MIGUU YOTE MIWILI BAADA YA TIMU KUPATA AJALI LEO ASUBUHI IKITOKEA MAZOEZINI MOSHI

   MSHAMBULIAJI Gerald Mathias Mdamu amevunjika miguu yote miwili baada ya kikosi cha Polisi Tanzania kupata ajali leo asubuhi kikitokea mazoezini Uwanja wa Chuo cha Polisi (TPC), Moshi mkoani Kilimanjaro. 
  Afisa Habari Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya Saa 5:00 asubuhi wakati timu ikitoka mazoezini kwenye uwanja wa TPC uliopo kwenye Kiwanda cha sukari na kusababisha wachezaji 16 kuumia na kulazwa hospitali ya KCMC.
  Pamoja na Mdamu aliyeumia zaidi na kuvunjika miguu yote miwili, wengine ni Abdulazizi Makame, Pius Buswita, Daruweshi Saliboko, Deusdedit Cossmas, Salum Ally, Abdulmalik Adam, Idd Mobby, Marcel Kaheza, Shaaban Stambuli, Yahaya Mbegu, Datus Peter, Mohammed Bakari, Mohammed Yusuph, Kassim Haruna na Christopher John.

  Pole Gerald Mathias Mdamu. Mungu akujaalie upone na kusimama tena.

  Wengine ni madereva George Mketo na Vicente Ngonyani na wachezaji wote wapo KCMC wakiendelea na uchunguzi wa daktari, chanzo cha ajali kinachunguzwa.
  Polisi imekutwa na janga hilo ikiwa katika maandalizi ya mechi zake za mwishoni za Ligi Kuu inayoelekea ukingoni.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI WA POLISI TANZANIA AVUNJIKA MIGUU YOTE MIWILI BAADA YA TIMU KUPATA AJALI LEO ASUBUHI IKITOKEA MAZOEZINI MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top