• HABARI MPYA

  Wednesday, July 07, 2021

  ITALIA YAING’OA HISPANIA KWA MATUTA NA KUTINGA FAINALI EURO

   ITALIA imetinga fainali ya Euro 2020 kwa ushindi wa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 dhidi ya Hispania usiku wa Jumanne Uwanja wa Wembley Jijiji London, England.
  Nyota wa Juventus, Federico Chiesa alianza kuifungia Italia dakika ya 60 akimalizia pasi ya mshambuliaji mwingine, Ciro Immobile wa Lazio kabla ya mtokea benchi, Alvaro Morata wa Juventus kuisawazishia Hispania dakika ya 80 akimalizia pasi ya kiungo wa RB Leipzig, Daniel Olmo.
  Na katika mikwaju ya penalti Olmo na Morata walikosa, huku Gerard Moreno na Thiago Alcantara pekee wakifunga kwa upande wa Hispania, wakati Andrea Belotti, Leonardo Bonucci, Federico Bernardeschi na Jorginho waliifungia Italia baada ya Manuel Locatelli kukosa ya kwanza.
  Olmo alipiga juu, ya Morata iliokolewa na kipa Gianluigi Donnarumma, wakati ya Locatelli pia iliokolewa na kipa Simon.
  Fainali ya Euro 2020 itachezwa Jumapili na Italia itakutana na mshindi wa mechi ya kesho baina ya England na Denmark.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ITALIA YAING’OA HISPANIA KWA MATUTA NA KUTINGA FAINALI EURO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top