• HABARI MPYA

  Friday, July 23, 2021

  DEPAY ATAMBULISHWA BARCA BAADA YA KUSAINI MIAKA MIWILI


  WINGA wa kimafaifa wa Uholanzi, Memphis Depay ametambulishwa Barcelona baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru kufuatia kumaliza mkataba wake
  Lyon ya Ufaransa. 
  Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyefurahi kujiunga na Barca acheze na Lionel Messi, anakwenda kufanya kazi tena na kocha Ronald Koeman, ambaye amewahi kumfundisha katika timu ya taifa ya Uholanzi.
  Na anakuwa mchezaji mpya wa nne kusajiliwa na vigogo hao wa Hispania baada ya Sergio Aguero na Eric Garcia, amabo pia wametua Camp Nou kama wachezaji huru kufuatia kuondoka Manchester City, na Emerson Royal.
  Mchezaji huyo wa zamani wa PSV na Manchester United amelazimika kukubali mshahara pungufu kwa asilimia 30, yaani kutoka kulipwa Pauni Milioni 7 hadi Milioni 5.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DEPAY ATAMBULISHWA BARCA BAADA YA KUSAINI MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top