• HABARI MPYA

  Thursday, July 15, 2021

  BIASHARA UNITED YAJIHAKIKISHIA KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AFRIKA MSIMU UJAO BAADA YA SARE YA 1-1 NA TANZANIA PRISONS LEO SUMBAWANGA

  TIMU ya Biashara United imejihakikishia kucheza Kombe la Shirikisho la Afrika msimu ujao baada ya sare ya 1-1 na wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

  Christian Zigah alianza kuwafungia Biashara United dakika ya 47, kabla ya Mohammed Mkopi kuisawazishia Tanzania Prisons dakika ya 56.
  Kwa sare hiyo, Biashara United imefikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 33 na kujihakikishia kumaliza nafasi ya nne, nyuma ya Azam FC yenye pointi 65, Yanga SC pointi 73 na Simba SC ambao ni mabingwa tayari kwa mara ya nne mfululizo wenye ponti 80 kuelekea mechi za mwisho Jumapili.
  Msimu ujao, bingwa na mshindi wa pili watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na mshindi wa tatu na wan ne watacheza Kombe la Shirikisho.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YAJIHAKIKISHIA KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AFRIKA MSIMU UJAO BAADA YA SARE YA 1-1 NA TANZANIA PRISONS LEO SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top